Sera ya Faragha
Ilisasishwa mwisho: Novemba 2026
Agiza Chakula inatilia maanani faragha yako. Sera hii inaeleza ni taarifa gani tunazokusanya, jinsi tunavyozitumia, na haki zako.
1. Taarifa Tunazokusanya
Tunakusanya taarifa unazotupatia kwenye tovuti na app ya simu: jina, namba ya simu, email (si lazima), mahali pa kuletea, oda zako na nyota/maoni unayotoa. Ukiruhusu, tunatumia mahali ulipo kuonyesha wauzaji wa karibu na kujaza mahali pa kuletea. Kwa wauzaji pia: picha za vyakula, maelezo ya biashara, na mahali walipo wakiwa kazini (ili mteja afuatilie oda). Namba ya kulipia inatumika kwa malipo ya simu.
2. Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako
Tunatumia taarifa zako kuunganisha na watoa huduma wa karibu, kukamilisha na kufuatilia oda, kupokea malipo na kuwalipa wauzaji, kutuma code za SMS za kuthibitisha na taarifa muhimu, kuboresha huduma, na kukulinda dhidi ya matumizi mabaya. Hatutumii taarifa zako kwa matangazo ya makampuni mengine.
3. Kushiriki Taarifa
Hatuuzi taarifa zako. Tunashiriki taarifa muhimu tu: na mtoa huduma au mgahawa wa oda yako (jina, namba, mahali pa kuletea); na PigaPay (PigaTech) kwa malipo ya simu na kutuma pesa kwa wauzaji; na mtoa huduma wa SMS kwa code za kuthibitisha. Kwenye app, kipengele cha kuscan QR code kinatumia ML Kit ya Google, inayotuma Google taarifa za kifaa na utendaji (kama aina ya simu) kwa ajili ya kuboresha huduma; picha ya kamera haitumwi popote. Taarifa kwenye simu (oda mpya, malipo) zinatumwa kupitia Firebase ya Google, inayotumia namba maalum ya simu yako kwa ajili hiyo tu; unaweza kuzizima kwenye Akaunti.
4. Usalama wa Taarifa
Tunatumia teknolojia za kisasa kulinda taarifa zako: mawasiliano yote yanapitia HTTPS na maneno ya siri yanahifadhiwa kwa njia isiyosomeka (hash). Hata hivyo, hakuna mfumo ulio salama kwa asilimia 100 mtandaoni.
5. Haki Zako
Una haki ya kuona, kusahihisha au kufuta taarifa zako. Unaweza kufuta akaunti yako mwenyewe kwenye app (Akaunti > Futa akaunti) au tovuti (Mipangilio > Usalama > Futa akaunti); maelezo yote yako kwenye ukurasa wa Futa Akaunti (/delete-account). Kumbukumbu za oda zinabaki bila jina lako kwa ajili ya hesabu na sheria.
6. Mawasiliano
Kama una maswali kuhusu sera hii, wasiliana nasi kupitia email: privacy@agizachakula.com